WIZARA YA ELIMU NA
MAFUNZO YA UFUNDI STADI
CHUO CHA UALIMU
KOROGWE
NGUZO ADILI ZA CHUO
1.Kibali cha kulala nje ya chuo, kumtembelea
mwanachuo asiye wa jinsia yake bwenini, kutoka nje ya mipaka ya chuo, ua
nyumbani kwa mfanyakazi hutolewa na mkuu wa chuo.
2.Kila
mwanachuo sharti awahi darasani, mstarini, bwaloni/ukumbini, katika kazi za
nje, mara aitwapo kwa kengele. Ni marufuku kwa mwanachuo kulala bwenini bila ya
kibali cha mwadili na mganga wa chuo.
3.Ni
marufuku kwa mwanachuo kumpotezea mwanachuo mwenzake muda katika mambo yasiyo
na msingi hasa mikutano isiyo rasmi, vikao vya gizani, ulevi wa pombe,
uasherati, bangi, madawa ya kulevya, kuishi kama mtu na mpenzi wake, kuasi na
kukiuka taratibu za chuo.
4. Mwanachuo
hatajishirikisha katika siasa wakati wote wa mafunzo yake hapa chuoni,
anatakiwa kila wakati kutumia busara katika kufanya maamuzi yake, kutimiza
wajibu kama utakavyoelekezwa na uongozi pamoja na wafanyakazi wengine wa chuo
na uongozi wa serikali ya wanachuo, na kufuata kanuni na taratibu zote za serikali
ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
5.Mwanachuo
hatakashifu, kuzomea, au kuguna wakati viongozi wa aina zote wa ndani na nje ya
chuo wanapozungumza bali atauliza swali ili aelezwe zaidi, unapaswa kujiheshimu
mwenyewe, kuwaheshimu wenzako, wakufunzi, wafanyakazi wengine pamoja na watu
wengine utakaokutana nao. Jizuie kufanya jambo lolote litakaloleta tafsiri ya
kuwadharau wengine.
6. Madai
yote ya mwanachuo kutaka kubadili dini au jina akiwa chuoni hayatakubalika.
7. Mwanachuo
atahudhuria masomo na vipindi vyote vya kujisomea na kufanya majaribio na
mitihani yote ya chuo, kanda na taifa kwa bidii, utulivu, juhudi na maarifa.
8.Kwa
usalama wa chuo ni marufuku kwa mwanachuo yoyote kupika bwenini au kukutwa na
vifaa vyovyote vinavyoweza kuleta hatari ya moto bwenini kama vile jila la
mafuta ya taa au umeme, heater, sufuria, pressure cookers n.k. Wanachuo wote
wanapaswa kuondoka madarasani saa 4:30 usiku.
9.Mwanachuo
atawapokea rasmi wageni wake kutoka ofisi ya zamu na kuwaelekeza taratibu za
chuo zinazowahusu. Mwanachuo atabeba lawama zote endapo itabainika kuwa
amesababisha matatizo au atakiuka taratibu za chuo.
10.Kila
mwanachuo anatazamiwa kujipenda, kuwa na maarifa na moyo wa kujituma, kutunza
mali ya serikali, chuo na watu wengine. Kuvaa mavazi ya heshima na safi wakati
wote, kutunza nywele vizuri, kutonyoa kipara, kufuga ndevu na sharafa, kuacha
kucha ndefu na kuvaa mapambo yasiyoruhusiwa.
11.Mwanachuoharuhusiwi kuwa na mimba akiwa chuoni au kuja
na mimba chuoni. Wanachuo wote yawapasa kuishi kama ndugu au kama kaka na dada
hairuhusiwi kugombana au kupigana wakati wote wa mafunzo, ndani na nje ya chuo
utapata kibali cha kutoka nje ya chuo na hataaibisha jina zuri la chuo kwa
kuonekana kwenye majumba ya starehe na nyumba za kulala wageni
Mimi
……………………………………………………………………. Nakubaliana na nguzo adili zote za chuo. Naahidi
kuzifuata kwa kipindi chote cha mafunzo yangu.
Sahihi
…………………………………………………. Tarehe
…………………………………………………………